Mfahamu Mtu Mwenye Umri Mkubwa Zaidi Duniani Aliye Hai
KIKONGWE
Kane Tanaka ndiye mwanamke anayetambuliwa kuwa na umri mkubwa zaidi duniani
aliye hai. Hii ni kulingana na kitabu cha Rekodi za Ulimwenguni za Guinness.
Tanaka
raia wa Japan alizaliwa Januari 2, 1903. Kwa sasa ana umri wa miaka 117 na
zaidi ya siku 266 mpaka leo Alhamisi.
Awali,
Wizara ya Afya, Kazi na Ustawi wa Jamii ilisema rekodi ya nyuma ilikuwa
inashikiliwa na mwanamke mwingine Mjapan, Nabi Tajima, kutoka Kisiwa cha
Kikai kilicho kusini-magharibi mwa Japan, ambaye alifariki Aprili 2018.
Tanaka,
ambaye ni mtoto wa saba miongoni mwa tisa, ni nesi katika jiji la Fukuoka
na Machi mwaka jana alitunukiwa zawadi ya kuwa binadamu mwenye umri mrefu zaidi
anayeishi.
Mwanamke
wenye umri mkubwa zaidi aliyewahi kuishi ni Jeanne Calment wa Ufaransa
aliyeishi miaka 122 na siku 164 ambapo mwanamme aliyeishi umri mkubwa zaidi
alikuwa Jiroemon Kimura wa Japan, aliyezaliwa Aprili 19, 1897
akafariki akiwa na umri wa miaka 116 na siku 54, siku ya Juni 12, 2013. HII
NI WIXMEDIA
ENDELEA KUTUFATILIA YOUTUBE
TUNAPATIKANA KAMA WIX MEDIA