RUDI MAMA (SIMULIZI)

 RUDI MAMA (SEHEMU YA KWANZA)

MWL JOSHUA

0622186752  WHATSAPP/SMS/CALL

Helen alilia kwa uchungu huku akimshika mama yake begani akisema

`` Mama amka mama amka ‘’

Helen aliita na kupiga kelele kwa takribani dakika kumi na tano bila mafanikio yoyote ,Mama  Helen alikuwa tayari ameshaaga dunia muda mrefu

Ilikuwa siku ya jumamosi  mama Helen aliamka mapema sana saa kumi za asubuhi alikuwa tayari amekwisha amka ,alipoamka hakuona sababu ya kumwamsha binti yake Hellen kwani alijua atamtoa kwenye usingizi ,cha zaidi alichokifanya alimsogelea na kumbusu kisha alimwongezea blanketi alilokuwa amelalia yeye ,baada ya hapo aliondoka kwa kunyata kutoka nje

Akiwa anatoka nje alikurupushwa na sauti ya mume wake aitwae Erick

``W ewe  mwanamke unaenda wapi sasa hivi wewe ‘’

Erick alikuwa amelala chini sakafuni akiwa amelewa chakari ,baada ya kurejea kutoka matembezini saa saba za usiku

Mama Helen hakuwa na muda wa kujibizana na mume wake kwani alikuwa akimchukulia kama mwendawazimu ,hajawai kuleta chochote katika familia ile kodi ya nyumba inalipwa na  mkewe ,matumizi ya nyumbani ,kusomesha mtoto kila kitu kilikuwa kinafanywa  na mama Helen, Erick kazi yake kubwa ilikuwa ni kulewa tu na kuzunguka mara nyingine alikuwa akiiba hadi hela za mkewe na kuzitumia kwa mambo yake bila hata huruma

Mama heleni alikuwa akijishughulisha na biashara ya nguo za mtumba alipata umaarufu mkubwa sana kutokana na kazi yake kila mtu alikuwa akimjua,kazi yake hiyo ilimwezesha mambo mengi sana aliweza kumsomesha mwanae hellen mpaka sasa Hellen yupo la tano gharama zote za shule matunzo ni mama ,jambo ambalo lilimfanya Hellen kumpenda sana mama yake na kumthamini ,Hellen alivalishwa kama ua alipendeza mno ukitegemea mama yake alikuwa muuza nguo,

Siku hiyo ya jumamosi majira ya saa kumi mama Hellen alichukuana na bodaboda wake na giza la asubuhi waliweza kuondoka bila kujali chochote kwani mama hellen alikuwa anaharaka sana ya kwenda kuwahi mzigo mpya uliokuwa ukitoka dubai

Upande wapi pili kulipambazuka Hellen aliamka mapema kabisa na kuangalia pembeni ya kitanda chake alipoona mama yake hayupo alipiga kitanda kwa hasira

``Mama bwana unaniboaga hapo tu umeondoka hata hujaniaga binti yako  jamani ‘’

Hellen alikimbia hadi sebuleni aliangalia picha ya mama yake iliyokuwa ukutani aliitoa na kuibusu kisha aliirudisha ,alipoangalia mezani aliona kimfuko kidogo ,alikifungua kwa haraka ,alikutana na barua

``Mwanangu nimewahi kazini pika chai utafunie na hizi sambusa usisahau kumwekea na baba yako ,ikifika mchana nimemwagiza Mama hapy atawaletea chakula mimi nitarudi usiku maana leo nitapitia na sokoni ,nakupenda mwanangu’’

Hellen alikuwa akipenda sana sambusa kwa haraka aliwasha jiko na kupika chai ,alimwekea  baba yake sambusa tatu na chai kisha alimsalimu na kumkaribisha ,Baba Hellen alisema

``Hahahah yaan we katoto una akili sana tena kazana ukue tupate mahari sawa ‘’

``Baba bwana ‘’  Hellen aliondoka huku akijisemea

``Yaan namshukuru mama maana huyu baba yangu akili zake zinamtosha mwenyewe’’

Ilipofika  Usiku……………………………………………………………..

Majira ya saa mbili usiku mama Hellen alikamilisha biashara zake  ,Siku hiyo alikuwa amepata faida kubwa kupita maelezo aliweza kuuza nguo zilizompatia faida ya shilingi elfu hamsini ,alikuwa na rah asana alijisemea

``Asante Mungu najua utanisaidia zaidi ya hapa nimlee mwanangu Hellen pamoja na familia yangu’’

Aliagiza boda boda kwa ajili ya kuelekea nyumbani

Siku hiyo ilikuwa siku ya ajabu kila kijana wa bodaboda aliyeitwa na mama Hellen alitoa kisingizio

Wengi walisema muda umekwenda wengine walisingizia umbali ,kutoka sokoni hadi nyumbani kwa mama Helen kulikuwa na kichochoro kirefu sana ambacho kiliwaogopesha wengi kwani sehemu hizo zilikuwa ni hatari kwa usalama

Mama hellen alishikwa na hofu sana baada ya  kuona saa tatu na nusu  imemkuta akiwa njiani ,aliamua kuchukua bajaji ambayo ilimpeleka na kumwacha njiani sehemu ambayo ingempasa kutembea kwa miguu

Mama Helen alivyoshushwa alianza kutembea kwa kukimbia   kwani kichochoro kile kilikuwa kimefunga sana ,kulikuwa na giza tororo pia kulikuwa  na sauti za kuogopesha

Mama Helen alikuwa akimwomba Mungu kimoyomoyo akisema ``Mungu nisaidie tu nifike salama nikamwone mwanangu najua ananingojea kwa hamu “

Alivyomaliza kuomba hivyo alisikia vishindo vya watu wakimfuatia

Mama hellen alikuwa ni mnene sana kwa umbile lake ila siku hiyo hakuamini wepesi ulitoka wapi ,alianza kukimbia kwa kasi sana ,alivyokuwa akikimbia alisikia sauti ikisema

``Wewe mama simama tutakufanya kitu mbaya ‘’

Mama hellen alikimbia sana huku akitetemeka,wakati wote alikuwa akisema

``Helen mwanangu ,Helen mwanangu ‘’

Alipata nguvu ya kukimbia hadi alifanikiwa kutoka katika uchochoro ule ,alipofika karibu na nyumbani kwao alipunguza mwendo huku akihema kwa nguvu na kusema

``Mungu wangu eeeee asante kwa kunivusha hapa’’

Alijilegeza kabisa na kutembea  kawaida ,akiwa anatembea alisikia vishindo vikimfuata ,alianza kupiga kelele za kuita watu kwa kuwa alikuwa ameshafika nje ya geti la nyumbani

Helen akiwa sebuleni akimsubiri mama yake kwa hamu ,kwake Helen hakuona chenye kumpa faraja ,Tv ilikuwa imeshamchosha alijikuta akimsubiri mama yake na kuangalia picha ya mama yake ukutani

Ndani ya dakika mbili mama Helen alizingirwa na vijana watatu ,walimsihi na kumwambia

``Toa kila ulicho nacho uondoke’’

Mama Helen aliwasihi kwa upole

``Nisameheni jamani  mimi ni mama yenu nalea sasa mnanikaba hivi mnajifutia laana wanangu’’

Wale vijana walikonyezana na kupeana ishara

Kijana mmoja alichomoa kirungu na kumtwanga mama Helen kichwan

``Pwaaaaaaa’’

Mama  Helen alitoa sauti moja tu ya mwisho

``Mungu wangu eeee Helen nakufa ‘’

Mama Helen alidondoka chini ,wezi wale waliondoka baada ya kumuua mama Helen na kumpora hela zake zote

Helen akiwa ndani alisikia sauti kama ya mama yake kwa haraka alifungua  geti na kutoka nje

Alipofika nje Helen hakuamini macho yake ,alimkuta mama yake akiwa amelala chini kwa mbali damu ilikuwa ikivuja kichwani

Helen alianza kupiga kelele

``Mama mamaaa eee amka mama ‘’

Helen alimshika bega mama yake na kuanza kumnyanyua ila alikuwa amelegea mwili mzima

Majiran walisogea sehemu ile ,kwa haraka walipogusa mapigo ya moyo walibaini ameshapoteza maisha kitambo

Helen alipoambiwa hakuamini alikuwa akimwita tu mama yake kwa nguvu

``Mamaaaaaa mama aaaaa’’

Kitendo hiki kiliwafanya watu watokwe na machozi .ndani ya dakika kumi Erick baba mzazi wa Helen alirejea kutoka katika pombe zake ,alipofika pale alishangazwa na alichokiona ,pombe zote zilikatika pale ,Erick alikuwa akimtegemea mkewe kwa kila kitu si chakula mavazi nk… Erick alipiga kelele ya nguvu

``Mke wanguuuu eee’’

Helen alimsogelea mama yake na kusema

``Mama jamani mama amka ulisema kesho jumapili tutaenda kwa bibi kumsalimu amka mama angu amka mama nitaenda na nani ,nitalala na nani ,nani atanisomesha mama mamaaa’’

Itaendeleaaa

Je Hellen atakuwa katika hali gani ,,,,,,,,,,,,,,,,,fuatilia

Simuliz hii ipo tayari unaweza isoma yote sasa  kwa sh 1000 




 

WIX MEDIA

This blog deal with art , musi

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

نموذج الاتصال